1 Kwa
maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye
kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja
itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
2 Lakini
kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika
mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini.
3 Nanyi
mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika
siku ile niifanyayo, asema Bwana wa majeshi.
4 Ikumbukeni
torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli
wote, naam, amri na hukumu.
5 Angalieni,
nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na
kuogofya.
6 Naye
ataigeuza...
MALAKI - SURA YA 3
1 Angalieni,
namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana
mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano
mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi.
2 Lakini
ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama
atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha,
ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo;
3 naye
ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi,
atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.
4 Wakati
ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za Bwana, kama
katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani.
5 Nami
nitawakaribieni ili kuhukumu; nami...
MALAKI - SURA YA 2
1 Na sasa,
enyi makuhani, amri hii yawahusu ninyi.
2 Kama
hamtaki kusikia, na kama hamtaki kuitia moyoni, ili kulitukuza jina langu,
asema Bwana wa majeshi, basi nitawapelekeeni laana, nami nitazilaani baraka
zenu; naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamyatii haya moyoni.
3 Angalieni,
nitaikemea mbegu kwa ajili yenu, nami nitapaka nyuso zenu mavi, naam, mavi ya
sadaka zenu; nanyi mtaondolewa pamoja nayo
4 Nanyi
mtajua ya kuwa mimi nimewapelekeeni amri hii, ili agano langu liwe na Lawi,
asema Bwana wa majeshi.
5 Agano
langu naye lilikuwa agano la uhai na amani; nami nikampa ili aogope, naye
akaniogopa, akalicha jina langu.
6 Sheria
ya kweli ilikuwa kinywani mwake, wala udhalimu haukuonekana midomoni mwake;
alikwenda pamoja nami...
MALAKI - SURA YA 1
1 Ufunuo
wa neno la Bwana kwa Israeli kwa mkono wa Malaki
2 Nimewapenda ninyi, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema,
Umetupendaje? Je! Esau siye ndugu yake Yakobo? Asema Bwana; ila nimempenda
Yakobo;
3 bali Esau nimemchukia na kuifanya milima yake kuwa ukiwa, na
urithi wake nimewapa mbweha wa nyikani.
4 Ijapokuwa Edomu asema, Tumepondwa-pondwa, lakini tutarudi na
kupajenga mahali palipoachwa hali ya ukiwa; Bwana wa majeshi asema hivi, Wao
watajenga, bali mimi nitaangusha; na watu watawaita, Mpaka wa uovu, na, Watu
ambao Bwana anawaghadhabikia milele.
5 Na macho yenu ninyi yataona, nanyi mtasema, Bwana ndiye mkuu
kupita mpaka wa Israeli.
6 Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi,
kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi...