AYUBU - SURA YA 23

1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, 
2 Hata leo mashitaka yangu yana uchungu; Pigo langu ni zito zaidi ya kuugua kwangu. 
3 Laiti ningejua mahali niwezapo kumwona, Nifike hata hapo anapokaa! 
4 Ningeiweka daawa yangu mbele yake, Na kukijaza kinywa changu hoja. 
5 Ningeyajua maneno atakayonijibu, Na kuelewa na hayo atakayoniambia. 
6 Je! Angeshindana nami kwa ukuu wa uwezo wake? La, lakini angenisikiliza. 
7 Hapo walekevu wangepata kuhojiana naye; Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele. 
8 Tazama, naenda mbele, wala hayuko; Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona; 
9 Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona; Hujificha upande wa kuume, hata nisimwone. 
10 Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. 
11 Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka. 
12 Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu, 
13 Lakini yeye ni mmoja, ni nani awezaye kumgeuza? Tena nafsi yake ilitakalo, ndilo afanyalo. 
14 Kwani yeye hulitimiliza hilo nililoamuriwa; Tena mambo mengi kama hayo ya pamoja naye. 
15 Kwa hiyo naona taabu mbele ya uso wake; Nitakapofikiri, namwogopa. 
16 Kwani Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia, Naye Mwenyezi amenitaabisha; 
17 Maana sikufadhaishwa kwa sababu ya giza, Wala kwa sababu giza kuu limenifunika uso.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii