AYUBU - SURA YA 25

1 Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema, 
2 Enzi na hofu zi pamoja naye; Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka. 
3 Je! Majeshi yake yahesabika? Ni nani asiyetokewa na mwanga wake? 
4 Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu? Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke? 
5 Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake; 
6 Siuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii