1 Wakashuka
watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama
desturi ya Musa hamwezi kuokoka.
2 Basi
baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu
wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda
Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo.
3 Basi,
wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria,
wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.
4 Walipofika
Yerusalemu wakakaribishwa na kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo
yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.
5 Lakini
baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima
kuwatahiri na kuwaagiza kuishika torati ya Musa.
6 Mitume
na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo.
7 Na
baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya
kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa
walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini.
8 Na
Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile
kama alivyotupa sisi;
9 wala
hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani.
10 Basi
sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo
baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua.
11 Bali
twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.
12 Basi
mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paulo wakiwapasha habari za
ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa.
13 Na
hao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akisema, Ndugu zangu, nisikilizeni.
14 Simeoni
ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika
hao kwa ajili ya jina lake.
15 Na
maneno ya manabii yapatana na hayo, kama ilivyoandikwa,
16 Baada
ya mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka.
Nitajenga tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha;
17 Ili
wanadamu waliosalia wamtafute Bwana, Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa
kwao;
18 Asema
Bwana, ajulishaye hayo tangu milele.
19 Kwa
sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika
Mataifa;
20 bali
tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama
zilizosongolewa, na damu.
21 Kwa
maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji
husomwa kila sabato katika masinagogi.
22 Basi
ikawapendeza mitume na wazee na kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na
kuwapeleka Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba; nao ni hawa, Yuda aliyeitwa
Barsaba, na Sila, waliokuwa watu wakuu katika ndugu. Wakaandika hivi na
kupeleka kwa mikono yao,
23 Mitume
na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa
Mataifa; Salamu.
24 Kwa
kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbua kwa maneno yao,
wakipotosha roho zenu, ambao sisi hatukuwaagiza;
25 sisi
tumeona vema, hali tumepatana kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwapeleka
kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo,
26 watu
waliohatirisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
27 Basi
tumewatuma Yuda na Sila, watakaowaambia wenyewe maneno yayo hayo kwa vinywa
vyao.
28 Kwa
maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo
lazima,
29 yaani,
mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama
zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.
30 Hata
hao wakiisha kupewa ruhusa wakatelemkia Antiokia; na baada ya kuwakusanya jamii
yote wakawapa ile barua.
31 Nao
walipokwisha kuisoma wakafurahi kwa ajili ya faraja ile.
32 Tena
Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno
mengi, wakawathibitisha.
33 Na
wakiisha kukaa huko muda, wakaruhusiwa na ndugu waende kwa amani kwa hao
waliowatuma. [
34 Lakini
Sila akaona vema kukaa huko.]
35 Na
Paulo na Barnaba wakakaa huko Antiokia, wakifundisha na kulihubiri neno la
Bwana, pamoja na watu wengine wengi.
36 Baada
ya siku kadha wa kadha Paulo akamwambia Barnaba, Haya! Mrejee sasa
tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno la Bwana, wa hali
gani.
37 Barnaba
akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao.
38 Bali
Paulo hakuona vema kumchukua huyo aliyewaacha huko Pamfilia, asiende nao
kazini.
39 Basi
palitokea mashindano baina yao hata wakatengana. Barnaba akamchukua Marko
akatweka kwenda Kipro.
40 Lakini
Paulo akamchagua Sila, akaondoka, akiombewa na wale ndugu apewe neema ya Bwana.
41 Akapita
katika Shamu na Kilikia akiyathibitisha makanisa.