ZABURI - SURA YA 126

1 Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto. 
2 Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu. 
3 Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi. 
4 Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini. 
5 Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. 
6 Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii