ZABURI - SURA YA 3

1 Bwana, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia, 
2 Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu. 
3 Na Wewe, Bwana, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. 
4 Kwa sauti yangu namwita Bwana Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. 
5 Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa Bwana ananitegemeza. 
6 Sitayaogopa makumi elfu ya watu, Waliojipanga juu yangu pande zote. 
7 Bwana, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki. 
8 Wokovu una Bwana; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii