ZABURI - SURA YA 47

1 Enyi watu wote, pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe. 
2 Kwa kuwa Bwana Aliye juu, mwenye kuogofya, Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote. 
3 Atawatiisha watu wa nchi chini yetu, Na mataifa chini ya miguu yetu. 
4 Atatuchagulia urithi wetu, Fahari ya Yakobo ambaye alimpenda. 
5 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti ya baragumu. 
6 Mwimbieni Mungu, naam, imbeni; Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni. 
7 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa akili. 
8 Mungu awamiliki mataifa, Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu. 
9 Wakuu wa watu wamekusanyika, Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu. Maana ngao za dunia zina Mungu, Ametukuka sana.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii