ZABURI - SURA YA 54

1 Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe, Na kwa uweza wako unifanyie hukumu. 
2 Ee Mungu, uyasikie maombi yangu, Uyasikilize maneno ya kinywa changu. 
3 Kwa maana wageni wamenishambulia; Watu watishao wananitafuta nafsi yangu; Hawakumweka Mungu mbele yao. 
4 Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia; Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu. 
5 Atawarudishia adui zangu ubaya wao; Uwaangamize kwa uaminifu wako. 
6 Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu; Ee Bwana, nitalishukuru jina lako, maana ni jema. 
7 Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu; Na jicho langu limeridhika Kwa kuwatazama adui zangu.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii