ZABURI - SURA YA 61

1 Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu. 
2 Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. 
3 Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate. 
4 Nitakaa katika hema yako milele, Nitaikimbilia sitara ya mbawa zako 
5 Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu. Umewapa urithi wao waliogopao jina lako. 
6 Utaziongeza siku za mfalme, Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi. 
7 Atakaa mbele za Mungu milele, Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi. 
8 Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii