ZABURI - SURA YA 63

1 Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji. 
2 Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako. 
3 Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu. 
4 Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu. 
5 Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha. 
6 Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku. 
7 Maana Wewe umekuwa msaada wangu, Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia. 
8 Nafsi yangu inakuandama sana; Mkono wako wa kuume unanitegemeza. 
9 Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiharibu, Wataingia pande za nchi zilizo chini. 
10 Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga, Watakuwa riziki za mbwa-mwitu. 
11 Bali mfalme atamfurahia Mungu, Kila aapaye kwa Yeye atashangilia, Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii