ZABURI - SURA YA 67

1 Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake. 
2 Njia yake ijulike duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote. 
3 Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru. 
4 Mataifa na washangilie, Naam, waimbe kwa furaha, Maana kwa haki utawahukumu watu, Na kuwaongoza mataifa walioko duniani. 
5 Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru. 
6 Nchi imetoa mazao yake MUNGU, Mungu wetu, ametubariki. 
7 Mungu atatubariki sisi; Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii