ZABURI - SURA YA 75

1 Ee Mungu, twakushukuru. Twakushukuru kwa kuwa Jina lako li karibu; Watu huyasimulia matendo yako ya ajabu. 
2 Nitakapoufikia wakati ulioamriwa, Mimi nitahukumu hukumu za haki. 
3 Ingawa dunia na wote wakaao humo wataharuki, Mimi mwenyewe nimezisimamisha nguzo zake. 
4 Naliwaambia waliojivuna, Msijivune; Na wasio haki, Msiiinue pembe. 
5 Msiiinue pembe yenu juu, Wala msinene kwa shingo ya kiburi. 
6 Maana siko mashariki wala magharibi, Wala nyikani itokako heshima. 
7 Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu. 
8 Maana mkononi mwa Bwana mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa. 
9 Bali mimi nitatangaza matendo yako milele, Nitamwimbia Mungu wa Yakobo. 
10 Pembe zote za wasio haki nitazikata, Na pembe za mwenye haki zitainuka.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii