ZABURI - SURA YA 8

1 Wewe, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni; 
2 Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi. 
3 Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha; 
4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? 
5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; 
6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. 
7 Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni; 
8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini. 
9 Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii