ZABURI - SURA YA 82

1 Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu. 
2 Hata lini mtahukumu kwa dhuluma, Na kuzikubali nyuso za wabaya? 
3 Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara; 
4 Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu. 
5 Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika. 
6 Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia. 
7 Lakini mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu. 
8 Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana Wewe utawarithi mataifa yote.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii