ZABURI - SURA YA 98

1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. 
2 Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake. 
3 Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. 
4 Mshangilieni Bwana, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. 
5 Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi. 
6 Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana. 
7 Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake. 
8 Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha. 
9 Mbele za Bwana; Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa adili.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii