ZABURI - SURA YA 114

1 Haleluya. Israeli alipotoka Misri, Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni. 
2 Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake. 
3 Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma. 
4 Milima iliruka kama kondoo waume, Vilima kama wana-kondoo. 
5 Ee bahari, una nini, ukimbie? Yordani, urudi nyuma? 
6 Enyi milima, mruke kama kondoo waume? Enyi vilima, kama wana-kondoo? 
7 Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana, Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo. 
8 Augeuza mwamba kuwa ziwa la maji, Jiwe gumu kuwa chemchemi.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii