1 Akawaambia
wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja
kwa sababu yake!
2 Ingemfaa
zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini,
kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.
3 Jilindeni;
kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.
4 Na
kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema,
Nimetubu, msamehe.
5 Mitume
wakamwambia Bwana, Tuongezee imani.
6 Bwana
akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu
huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.
7 Lakini,
ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng'ombe, atakayemwambia mara
arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula?
8 Je!
Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe
kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa?
9 Je!
Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa?
10 Vivyo
hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa
wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.
11 Ikawa
walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na
Galilaya.
12 Na
alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama
mbali,
13 wakapaza
sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!
14 Alipowaona
aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda
walitakasika.
15 Na
mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti
kuu;
16 akaanguka
kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
17 Yesu
akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?
18 Je!
Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?
19 Akamwambia,
Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.
20 Na
alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia,
ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza;
21 wala
hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo
ndani yenu.
22 Akawaambia
wanafunzi, Siku zitakuja mtakapotamani kuona siku moja katika siku zake Mwana
wa Adamu, msiione.
23 Tena
watawaambia, Tazama, kule! Tazama, huku! Msiondoke mahali mlipo, wala
msiwafuate;
24 kwa
kuwa, kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hata upande
huu chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake.
25 Lakini
kwanza, hana budi kupata mateso mengi, na kukataliwa na kizazi hiki.
26 Na
kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa
Adamu.
27 Walikuwa
wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia
katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.
28 Na
kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa,
walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga;
29 lakini
siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni
vikawaangamiza wote.
30 Hivyo
ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.
31 Katika
siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili
kuvitwaa; na kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma.
32 Mkumbukeni
mkewe Lutu.
33 Mtu
ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza
ataiponya.
34 Nawaambia,
usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja
ataachwa.
35 Wanawake
wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
36 Watu
wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.]
37 Wakajibu,
wakamwuliza, Wapi, Bwana? Akawaambia, Ulipo mzoga, ndipo watakapokutanika tai.