ZABURI - SURA YA 112

1 Haleluya. Heri mtu yule amchaye Bwana, Apendezwaye sana na maagizo yake. 
2 Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. 
3 Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele. 
4 Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. 
5 Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki. 
6 Kwa maana hataondoshwa kamwe; Mwenye haki atakumbukwa milele. 
7 Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana. 
8 Moyo wake umethibitika hataogopa, Hata awaone watesi wake wameshindwa. 
9 Amekirimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu. 
10 Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuyeyuka, Tamaa ya wasio haki itapotea.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii