ZABURI - SURA YA 113

1 Haleluya. Enyi watumishi wa Bwana, sifuni, Lisifuni jina la Bwana. 
2 Jina la Bwana lihimidiwe Tangu leo na hata milele. 
3 Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la Bwana husifiwa. 
4 Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote, Na utukufu wake ni juu ya mbingu. 
5 Ni nani aliye mfano wa Bwana, Mungu wetu aketiye juu; 
6 Anyenyekeaye kutazama, Mbinguni na duniani? 
7 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani. 
8 Amketishe pamoja na wakuu, Pamoja na wakuu wa watu wake. 
9 Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii