ZABURI - SURA YA 120

1 Katika shida yangu nalimlilia Bwana Naye akaniitikia. 
2 Ee Bwana, uiponye nafsi yangu Na midomo ya uongo na ulimi wa hila. 
3 Akupe nini, akuzidishie nini, Ewe ulimi wenye hila? 
4 Mishale ya mtu hodari iliyochongoka, Pamoja na makaa ya mretemu. 
5 Ole wangu mimi! Kwa kuwa nimekaa katika Mesheki; Na kufanya maskani yangu Katikati ya hema za Kedari. 
6 Nafsi yangu imekaa siku nyingi, Pamoja naye aichukiaye amani. 
7 Mimi ni wa amani; Bali ninenapo, wao huelekea vita.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii