ZABURI - SURA YA 121

1 Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? 
2 Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi. 
3 Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye; 
4 Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli. 
5 Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume. 
6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku. 
7 Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. 
8 Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii