ZABURI - SURA YA 124

1 Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa, 
2 Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Wanadamu walipotushambulia. 
3 Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu 
4 Papo hapo maji yangalitugharikisha, Mto ungalipita juu ya roho zetu; 
5 Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu Maji yafurikayo. 
6 Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao. 
7 Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka. 
8 Msaada wetu u katika jina la Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii