ZABURI - SURA YA 129

1 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Israeli na aseme sasa, 
2 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Lakini hawakuniweza. 
3 Wakulima wamelima mgongoni mwangu, Wamefanya mirefu mifuo yao. 
4 Bwana ndiye mwenye haki, Amezikata kamba zao wasio haki. 
5 Na waaibishwe, warudishwe nyuma, Wote wanaoichukia Sayuni. 
6 Na wawe kama majani ya darini Yanyaukayo kabla hayajamea. 
7 Ambayo mvunaji haujazi mkono wake, Wala mfunga miganda kifua chake. 
8 Wala hawasemi wapitao, Amani ya Bwana ikae nanyi, Twawabariki kwa jina la Bwana.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii