ZABURI - SURA YA 130

1 Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia. 
2 Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu. 
3 Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? 
4 Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe. 
5 Nimemngoja Bwana, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia. 
6 Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi. 
7 Ee Israeli, umtarajie Bwana; Maana kwa Bwana kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi. 
8 Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii