ZABURI - SURA YA 142

1 Kwa sauti yangu nitamlilia Bwana, Kwa sauti yangu nitamwomba Bwana dua. 
2 Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, Shida yangu nitaitangaza mbele zake. 
3 Nilipozimia roho uliyajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego. 
4 Utazame mkono wa kuume ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho. 
5 Bwana, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai. 
6 Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye nao wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi. 
7 Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii