ZABURI - SURA YA 29

1 Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu; 
2 Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu. 
3 Sauti ya Bwana i juu ya maji; Mungu wa utukufu alipiga radi; Bwana yu juu ya maji mengi. 
4 Sauti ya Bwana ina nguvu; Sauti ya Bwana ina adhama; 
5 Sauti ya Bwana yaivunja mierezi; Naam, Bwana aivunja-vunja mierezi ya Lebanoni; 
6 Airusha-rusha kama ndama wa ng'ombe; Lebanoni na Sirioni kama mwana-nyati. 
7 Sauti ya Bwana yaipasua miali ya moto; 
8 Sauti ya Bwana yalitetemesha jangwa; Bwana alitetemesha jangwa la Kadeshi. 
9 Sauti ya Bwana yawazalisha ayala, Na kuifichua misitu; Na ndani ya hekalu lake Wanasema wote, Utukufu. 
10 Bwana aliketi juu ya Gharika; Naam, Bwana ameketi hali ya mfalme milele. 
11 Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii