ZABURI - SURA YA 30

1 Ee Bwana, nitakutukuza kwa maana umeniinua, Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu. 
2 Ee Bwana, Mungu wangu, Nalikulilia ukaniponya. 
3 Umeniinua nafsi yangu, Ee Bwana, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni. 
4 Mwimbieni Bwana zaburi, Enyi watauwa wake. Na kufanya shukrani. Kwa kumbukumbu la utakatifu wake. 
5 Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha. 
6 Nami nilipofanikiwa nalisema, Sitaondoshwa milele. 
7 Bwana, kwa radhi yako Wewe uliuimarisha mlima wangu. Uliuficha uso wako, Nami nikafadhaika. 
8 Ee Bwana, nalikulilia Wewe, Naam, kwa Bwana naliomba dua. 
9 Mna faida gani katika damu yangu Nishukapo shimoni? Mavumbi yatakusifu? Yataitangaza kweli yako? 
10 Ee Bwana, usikie, unirehemu, Bwana, uwe msaidizi wangu. 
11 Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; Ulinivua gunia, ukanivika furaha. 
12 Ili utukufu wangu ukusifu, Wala usinyamaze. Ee Bwana, Mungu wangu, Nitakushukuru milele.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii