ZABURI - SURA YA 87

1 Msingi wake upo Juu ya milima mitakatifu. 
2 Bwana ayapenda malango ya Sayuni Kuliko maskani zote za Yakobo. 
3 Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee Mji wa Mungu. 
4 Nitataja Rahabu na Babeli Miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi; Huyu alizaliwa humo. 
5 Naam, mintarafu Sayuni itasemwa, Huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye juu Ataufanya imara. 
6 Bwana atahesabu, awaandikapo mataifa, Huyu alizaliwa humo. 
7 Waimbao na wachezao na waseme, Visima vyangu vyote vimo mwako.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii