1 Basi,
kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika,
atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake
katika ulimwengu, aliwapenda upeo.
2 Hata
wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa
Simoni Iskariote, moyo wa kumsaliti;
3 Yesu,
hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa
Mungu naye anakwenda kwa Mungu,
4 aliondoka
chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni.
5 Kisha
akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa
kile kitambaa alichojifunga.
6 Hivyo
yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi?
7 Yesu
akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.
8 Petro
akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama
nisipokutawadha, huna shirika nami.
9 Simoni
Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa
changu pia.
10 Yesu
akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu
safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote.
11 Kwa
maana alimjua yeye atakayemsaliti; ndiyo maana alisema, Si nyote mlio safi.
12 Basi
alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena,
akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea?
13 Ninyi
mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.
14 Basi
ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo
kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.
15 Kwa
kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.
16 Amin,
amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu
kuliko yeye aliyempeleka.
17 Mkiyajua
hayo, heri ninyi mkiyatenda.
18 Sisemi
habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate
kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake.
19 Tangu
sasa nawaambia kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa mimi
ndiye.
20 Amin,
amin, nawaambieni, Yeye ampokeaye mtu ye yote nimpelekaye, anipokea mimi; naye
anipokeaye mimi; ampokea yeye aliyenipeleka.
21 Naye
alipokwisha kusema hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia akisema, Amin,
amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.
22 Wanafunzi
wakatazamana, huku wakiona shaka ni nani amtajaye.
23 Na
palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu
alimpenda.
24 Basi
Simoni Petro akampungia mkono, akamwambia, Uliza, ni nani amtajaye?
25 Basi
yeye, hali akimwelekea Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani?
26 Basi
Yesu akajibu, Ndiye mtu yule nitakayemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge,
akalitwaa akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote.
27 Na
baada ya hilo tonge Shetani alimwingia. Basi Yesu akamwambia, Uyatendayo
yatende upesi.
28 Wala
hakuna mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua sababu ya kumwambia hivyo.
29 Kwa
maana wengine walidhania, kwa kuwa Yuda huchukua mfuko, ya kwamba Yesu
alimwambia kama, Nunua mnavyovihitaji kwa sikukuu; au kwamba awape maskini
kitu.
30 Basi
huyo, akiisha kulipokea lile tonge, akatoka mara hiyo. Nako kulikuwa ni usiku.
31 Basi
huyo alipokwisha kutoka, Yesu alisema, Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, naye
Mungu ametukuzwa ndani yake.
32 Mungu
naye atamtukuza ndani ya nafsi yake; naye atamtukuza mara.
33 Enyi
watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta; na kama vile
nilivyowaambia Wayahudi ya kwamba, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja; kadhalika
sasa nawaambia ninyi.
34 Amri
mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo
hivyo.
35 Hivyo
watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo
ninyi kwa ninyi.
36 Simoni
Petro akamwambia, Bwana, unakwendapi? Yesu akamjibu, Niendako huwezi kunifuata
sasa; lakini utanifuata baadaye.
37 Petro
akamwambia, Bwana, kwa nini mimi nisiweze kukufuata sasa? Mimi nitautoa uhai
wangu kwa ajili yako.
38 Yesu
akamjibu, Je! Wewe utautoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia,
Jimbi hatawika hata wewe utakapokuwa umenikana mara tatu.