ZABURI - SURA YA 122

1 Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana. 
2 Miguu yetu imesimama Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu. 
3 Ee Yerusalemu uliyejengwa Kama mji ulioshikamana, 
4 Huko ndiko walikopanda kabila, Kabila za Bwana; Ushuhuda kwa Israeli, Walishukuru jina la Bwana. 
5 Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, Viti vya enzi vya mbari ya Daudi. 
6 Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao; 
7 Amani na ikae ndani ya kuta zako, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako. 
8 Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, Amani ikae nawe. 
9 Kwa ajili ya nyumba ya Bwana, Mungu wetu, Nikutafutie mema.

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii